Monday, July 29, 2013

NANDO NJE YA BBA

Katika kikao hicho uongozi wa Big Brother Africa ulimshutumu mshiriki wa Tanzania, Ammy Nando, kwa ugomvi alioufanya dhidi ya Elikem wa Ghana siku ya Ijumaa iliyopita. Ugomvi huo ulishuhudia wawili hao wakitukanana kwa maneno makali.
Nando ndiye aliyeanzisha ugomvi huo. Maneno makali na uchokozi ni mambo ambayo yamepigwa marufuku na sheria za Big Brother.
“Mshiriki yeyote ambaye ataanzisha ugomvi ataondolewa katika mjengo mara moja. Ugomvi ni pamoja na mtu kujidhuru mwenyewe au kuwadhuru watu wengine. Vilevile, madhara ni pamoja na kuwasumbua wengine, kuwalazimisha kufanya mambo wasiyoyataka na kuwaonea,” alisema mmoja wa maofisa wa mjengo huo aliyejulikana kama Biggie.
Katika msimu huu, Big Brother, imeweka sheria ya maonyo matatu ambayo yanatumika kwa washiriki iwapo watakiuka taratibu za shindano hilo. Kwa mujibu wa sheria hizo, Nando alikuwa tayari amepewa onyo la pili ambapo Elikem alipewa onyo la kwanza.
Baada ya mjadala huo, Mtanzania huyo aliitwa katika chumba cha maamuzi (Diary Room) ambako alipewa onyo la tatu kwa kuanzisha ugomvi huo dhidi ya Elikem ambapo alisema: “Najisikia kama nataka kumchoma kisu jamaa huyu. Mtu mweusi kama huyu (nigga) anastahili kufa.”
Zaidi ya hapo, Nando aliwahi kukamatwa akiwa amelala na mkasi chini ya kitanda chake, ambapo tukio hilo halikuwa la kwanza kwa mshiriki huyo kukamatwa akiwa na silaha katika mjengo huo. Mshiriki huyo kijana ambaye amekuwa katika mjengo huo kwa wiki tisa, mwezi uliopita alipewa onyo kali baada ya kukutwa akiwa na kisu wakati wa hafla ya Channel O Party.
Kuwa na silaha au kutaka kuanzisha vurugu katika mjengo huo, ni uvunjaji wa sheria za Big Brother.
Baada ya kikao hicho Nando aliambiwa aondoke katika mjengo huo mara moja ambapo washiriki wengine pia walipewa onyo la kuendesha mambo yao kama watu wazima.
Source: Sundayshomary.com


TanzaniaNando

1 comment:

  1. Jaman alikuwa ananikosha sana huyu!Basi sina hata hamu ya kuanagalia tena mashindano. Feza sina mzuka naye sana.

    ReplyDelete