Friday, July 26, 2013

Chile to Kili!

Takribani wiki imepita bila kupost chochote hapa. Ubize wa hapa na pale, ndio ulionitinda. Yako mambo mengi muhimu ya kuandikwa kila siku na kila wakati lakini  kutokana na kubanwa huku, n’takuwa n’napost kila n’napopata nafasi kama leo!
Story la leo inanirudisha nyuma kidogo.
Siku moja nikiwa Tanzania, kama kawaida yangu kufuatilia habari, nilipomaliza kutazama ile ya TBC1, nikatupia macho Star Tv.
Hapo nikakutana na matangazo ya BBC kwa lugha ya Kiswahili. Ilitangaz moja kwa moja kutokea London, nchini Uingereza. Studioni nikamwona mtangazaji, Salim Kikeke  akimuaga na kumkaribisha tena, kijana aliyezungumza Kiswahili huku pembeni yake ikiwa imepaki baiskeli. Akainuka. Akaiufuata baiskeli na kuikokota hadi nje ya studio.
Sikuwahi kipindi tangu mwanzo,kwa hiyo sikuelewa kilichomfanya kijana yule kuwa pale akihojiwa. Haraka haraka, nikajiamninisha kwambaa pengine ni mmoja kati ya washiriki wa mbio za kukimbizana kwa baiskeli na ile ilikuwa ni habari ya michezo!
Ila wakati maswali yananizidi uwezo, mdogo wangu aliyeifuatilia pia habari ile, akaniuliza,
“Mbona kama unashangaa bro, kulikoni? Au unamshangaa Lelo?”
“Lelo?” Nikamjibu kwa kumuuliza swali. “Lelo ni nani?”
 “Ni yule kijana uliyemwona anatoka na baiskeli pale!” akajibu na kuinuka. Akatokomoe huyo, chumbani.
Nikabaki mbele ya Tv peke yangu. Nilitaman kuendela kumwuliza ili anijuze mengi. Kiu ya haki ya ufahamu, ilishanikaba. Mara huyo. Anarudi kutoka chumbani. Mikono yake,imejaa laptop yake.
“Soma mtandao huu, niliufuatilia tangu jana!”
“Nilipoutazama nikakukana na www.chiletokili.com
Nikagundua safari ya maajabu!
Anaitwa Elvis Munisi, a.k.a Lelo, mzaliwa wa Tanzania. Ameamua kuzunguka dunia nzima kwa kutumia baiskeli yake, kutokea nchini Chile hadi mlima Kilimanjaro.
Lengo lake kuu, sio kutalii, bali ni kuchangisha pesa kwa ajli ya masomo ya mambo ya mazingira.
Usiku mzima nililala nikimfikiria Elvisi na kukumbuka maneno mengi ya wanafalsafa akiwemo Mahatma Gandhi aliyesema, “Be The Change You Want To See In The World’’ akimaansiha kwamba kuwa chanzo cha mabadliko kwa namna unavyoona dunia inapaswa iwe.
Elvis Munis pichani.

2 comments:

  1. Inabidi apigiwe makofi..napenda kutembelea baiskeli lakini huyu kiboko. Hongera na kila la heri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jambo alilofanya ni kubwa na la ajabu sana! Zaidi ya kupigiwa makofi, nadhani anafaa pia kuwekwa kwenye vitabu vya kumbukumbu za rekodi ya dunia!

      Delete