Swahili Abroad ni nin?

Ni blog kuhusu watanzania waishio nje ya Tanzania. Wanaafrika Mashariki wanaozungumza lugha ya Kiswahili walio ughaibuni, wanahusika pia. Hapa utapata makala zinazozungumzia maisha yao halisi, burudani, michezo, harakati za kimaisha, masomo, kazi, ubunifu, urembo pamoja na mengine mengi yanayowazunguka. Yeyote anayefanya mazuri kuhusu lugha hii, utamkuta hapa. Lengo  kuu ni kuwafanya Wanaafrika Mashariki waliobaki nyumbani kujifunza kutoka kwa walio ughaibuni yale yanayostahili kuwaletea maendeleo. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema, "hii ndio nyumba ya Kiswahili Ulimwenguni!"



3 comments:

  1. Hongera sana Kasyome,ila ningependa kama makala na habari zako uziandalia hata kipindi cha radio, uwe hata unatuwekea online au hata kwenye station yoyote inayosikika East Africa! Makala na habari hizi zina mvuto sana hasa kwa vijana wanaotafuta mafanikio, wanaweza kujifunza kutoka kwa ndugu au marafiki walioko nje.
    Sina mengi ila kutoa hongera zangu nyingi kwa kuanzisha blog hii.
    Mdau, Bombay, India.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana mdau.
      Nimeupokea ushauri wako.
      N'nakuomba uendelee kuipitia blog hii mara kwa mara ili uendelee kuapata zaidi ya ulichokipata leo!
      Asante sana.

      Delete
  2. iddi .h. wabusa nasema ndugu umenena kweli watanzania tupende lugha yetu atakama tupo nnje.

    ReplyDelete