Tuesday, June 11, 2013

Mtanzania mwingine afia Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa Zamani Ofisi ya Rais Ikulu, Mzee Timothy Apiyo (pichani chini), amefariki dunia katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini alikokuwa amelazwa. Marehemu Mzee Apiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kwa Kipindi kirefu mpaka alipostaafu na kuhamia Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Anatajwa kuwa ni mmoja wa viongozi waandamizi waliokuwa hawana masihara kazini, kiasi hata viongozi serikalini walikuwa wakimheshimu sana.

                     Rest In Peace

6 comments: