Sunday, June 16, 2013

Mtanzania na mavazi ya Kitanzania Sweden.

Kama ilivyo ada ya blog hii, daraja la mawasailiano ya wazi kati ya Wanaafrika Mashariki walio ughaibuni na waliobaki nyumbani, leo tunaye Mtanzania. Huyu anaishi nchini Sweeden, moja ya nchi zinazounda sehemu ya Scandinavia. Mazungumzo yetu yanajikita kugundua tofauti ya maisha halisi kati ya Sweden na Tanzania, hasa utamaduni na elimu.
Baada ya maamkizi, tukaanza mazungumzo kama ifuatavyo: Karibu msomaji,,,
“SA: Jina lako unaitwa nani?
AZIZA:Naitwa Aziza Issack.
SA:Unatokea mkoa gani?
AZIZA:Natokea Tanga.
SA:Umeingia nchini humo mwaka gani?
AZIZA:2009.
SA:Uliingia kimasomo au kuhamia?
AZIZA:Nilihamia kifamilia.
SA:Ok, unaishi mji gani?
AZIZA:Uppasla mtaa wa Solitvagen.
SA:Unasoma au unafanya kaz?
AZIZA:Nasoma.
SA:Unasomea nini.
AZIZA:Nasomea nursing.
SA:Chuo gani?
AZIZA:Lundellska.  
SA:Elimu ya Sweden na Tanzania unakotokea unaizungumziaje?
AZIZA:Kwanza tofauti ni kubwa sana maana huku mimi nilipofika siku ya kwanza niliona maajabu!
SA:Maajabu gani?
AZIZA:Elimu huku ni kama kazi, kila mwanafuzi unapohudhuria shule mwisho wa mwezi wapewa hela na ukihudhuria kidogo unakatwa! Ilinishangaza sana maana tz ni ndoto japokuwa tuna gesi na madini yanayoweza kuifanya nchi kufikia mfumo huu pia!
SA:Ok, hebu tuwaachie viongozi jambo hilo maana hapa sio mahala pake kuliongelea! Ukipewa nafasi ya kuutangaza utamaduni au utalii wa Tanzania,utaanza na lipi hasa?
AZIZA:Ntaanza na mavazi.
SA:Kwa nin mavazi?
AZIZA:Hapa mtaani kwangu na shule ninakosoma, kila nikivaa kitenge, wenyeji wanaonesha kushangaa sana na kuniuliza maswali mengi.
SA:Maswali kama ya aina gani?
AZIZA:Nakumbuka kuna siku nilivaa kitenge,  mmoja akaniuliza kuwa mimi ni Mnaijeria? Yeye alifahamu kuwa wanaijeria ndio huvaa vitenge maana amezoea kuwaona katika filamu. So maswali kama haya natamani kuyajibu kwa kuitangaza zaidi Tanzania.
SA:Kabla hatujamaliza mazungumzo yetu, una lipi la mwisho kwa msomaji?
AZIZA:Kwakweli ningependa kumalizia kwa kutoa ushauri kwa vijana wanaopenda kuja kusoma huku, wakaze buti na watafute nafasi ziaidi huku kwani mfumo wa elimu ni mzuri na hakuna ada!
SA:Ok, tunakushukuru kwa kutumia muda wako na tunakutakia mafanikio mema.
AZIZA:Asante, nami pia nashukuru sana na Mungu akubariki.”
Naam, msomaji huo ndio mwisho wa makala yetu, tulitazama maisha ya Sweden  kwa mtanzania huyu. Je, wewe ungependa kuzungumzia nin katika blog yetu? Usikae kimya,andika kwa moreinfoz@yahoo.com
Aziza akiwa katika moja ya maonesho ya mavazi ya Kizanzibar mwaka jana, shuleni kwake.
Aziza katika pozi la kidole mdomoni!

5 comments:

  1. hongera sana mdada, unatuwakilisha vyema watanzania, ila ongeza juhudi uanzishe hata kituo cha kufundisha Kiswahili huko,

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa yote...ila nataka niwe tofauti kidogo nawe hapo kwenye elimu ..ndiyo wanafunzi wanapata kwasababu hapa maisha ni gharama sana na hata chakula na ndiyo serikali inawasaidia kidogo. Kuhusu mavazi nakubaliana nawe ukivaa kitenge kanga wanapenda sana na ndiyo maana mara nyingi huwa nasema kwa nini tunapenda sana nguo za kutoka nchi nyingine wakati tuna nguo nzuri za asili?

    ReplyDelete
  3. kwa hiyo, hiyo nchi sio nzuri kama anavyoisifia? Unaposema unakuwa tofauti kwenye elimu, hebu mtupe taarifa sahihi, msituchanganye jaman, tunawategemea huko

    ReplyDelete
  4. Tofauti ni kwamba wanapopata zile pesa na sawa tu na mzazi kulipa ada ya mwanae. Nikisema hivi naamaanisha watu waote wanalipa kodi serikalini na pesa zile zile zinalipwa kwa wanafunzi. Na kodi walipayo si kidogo kila mwezi mshahara unakatwa. Na tena baadae mtu unalazimika kukopa ili kumaliza masomo hupewi pesa mpaka tamati ya masomo yako.

    ReplyDelete
  5. habari wa tz wezangu? nashukuru kwa ukarimu wenu kufatilia makala hii kwani bila nyie kusoma nakufatilia watz walio nchi za nje wanafanya nini haswa kutuwakilisha sie tulio bakia tz. ningependa tu ni jib kwaufasaha na ukarimu ilii muelewe nini nilichokizungumza zaidi sana kwenye elim....baisi makala nilijibu kama swali lilivyo ulizwa ila nitakuelezea kidogo ili utambue zaidi


    Elim ya sweden tofauti yake iko kubwa sana na tz ukiangalia swala zima la ADA huku hakuna, elimu ya hapa nibure kwavijana wote na iliwekwa sheria na gaverment ya sweden kuwa kila kijana anapo huzuria shuleni apewe hela hivyo basi kuifanya shule kwavijana iwe KAZI kuwa ukiwa unahuzuria shule unapewa mshahara na kwamauzurio uliyoo huzuria na hela hiyoo inazunguka kwa kila mtu anaye fanya kazi hapa basi ana sitahilii kulipa 33% yamshahara wake ili wanafunzi hao nao wapate wasiwe natamaa yakutoo acha shule nakukimbilia kufanya ufazui ninaposema ufazui ni maana hiyoo usiwe chokoraa wamta,mwenye tamaa za hela,na kwa wasichana tusijiuze mwili kupata hela. sizani ushanielewa ewe mtz mwezangu..........MI NINGEPETA UNITAFUTE NAUSISITE KUNIULIZA SWALI LOLOTE LILE LINALO KUZINGIRA NAKULIWAZA ETI WATZ wa ughaibuni wanafanya nn uliza na pia ningependa kukushukuru wee mwenye kunisaidia pale nilipo kosea kurekebishana nisehem ya maisha.
    asanteni MUNGU awabariki

    ReplyDelete