Mwanzo
wa makala zetu, tulianza kwa kuzungumza na MwanaAfrika Mashariki aishie nchini
Canada, akitokae Rwanda. Leo tunaye Mtanzania. Huyu anaishi Ujerumani, nchi ambayo
iko katika orodha ya nchi tajiri duniani. Karibu tuungane kwa mazungumzo haya…
“SA: Habari dada...!Janeth: Salama ndugu yangu, habari za huko…
SA: Huku kwema dada yangu. Naomba kuzungumza na wewe machache ya kimaendeleo kama hautajali.
Janeth: Jisikie huru mwaya..,
SA: Asante sana. Naomba kwa leo tukufahamu kwa ufupi, kisha siku zitakavyokuwa zinasonga mbele tutakuwa tukikushirikisha katika mada mbalimbali. Tunazungumza na nani kabla ya yote?
Janeth: Naitwa Janeth Pastor Mtonyi.
SA: Unatokea nchi gani?
Janeth: Tanzania.
SA: Mkoa gani?
Janeth: Dodoma.
SA: Dodoma kubwa!
Janeth: Ha! haaa! haaa! (Anacheka) Halafu wewe, swali lako limenipa burudani hadi nacheka! Eniwei natokea kijiji cha Mpunguzi kilomita 27 kutoka Dodoma mjini, njia ya kwenda Iringa.
SA: Ukiburudika kwa ajili yangu kwangu ni furaha zaidi maana nakuwa nimeshiriki katika kuongeza uhai wako! (Hapo na mimi nilicheka pia) Nimependa jibu lako ila sio nia yangu kukuchimba zaidi! Unaishi nchi gani kwa sasa?
Janeth: Naishi Ujerumani kaka.
SA: Mji gani?
Janeth: Karlsruhe!
SA: Haya naomba kujua tofauti ya mshahara unaopata hapo ukilinganisha na Tanzania, ili msomji wangu ambaye hajafika Ujerumani na angependa kuja kufanya kazi huko apate picha kamili.
Janeth: Kwanza kabla sijakujibu swali lako, kumbuka kuwa, kulinganisha uchumi wa Ujerumani na Tanzania au Afrika Mashariki kwa ujumla, inaweza kuwa sawa na kulinganisha usingizi na kifo!
SA: Kwa vipi? Ufafanuzi hapo tafadhari…!
Janeth: Ngoja nikupe, utakuta kwa mfano, mtu anafanya kazi inayomlipa laki moja na elfu ishirini pesa za kitanzania, kwa saa moja na anafanya kazi masaa 8 x 30! Tena Ujerumani ni moja kati ya nchi za kwanza kwa utajiri duniani, social system hata omba omba bado wanapewa pesa inazidi mshahara wa Dr. Tanzania!
SA: Hapo swali langu siwezi kuliuliza tena, maana utakuwa “umbulula”! Tuhamie swali lingine…! Kitaaluma wewe ni nani?
Janeth: Umeona eee…! Kitaaluma mimi ni Nurse.
SA: Ok,kwa Tanzania kabla haujawa Nurse ulipita shule gani?
Janeth: Nilisoma Kilimatinde.
SA: Mh! Hapo umejibu kwa kifupi sana ila sitajali! Enhee, baada ya Kilimatinde, ukaendeleaje?
Janeth: Baada ya pilikapilika za hapa na pale, nilihamia huku. Nikaendelea katika chuo cha Ulm College of Nursing , na kumiliki shahada ya kwanza ya Nursing Managemant!
SA: Hongera kwa kumiliki “nondo ya kutobolea umasikini Afrika”. Unaitumiaje elimu yako kuinufaisha pia Tanzania?
Janeth: Nina malengo mengi sana likiwemo la ujenzi wa Zahanati kijijini kwetu Mpunguzi, ambapo nitabase na watoto wadogo pamoja na wazee wasiojiweza. Pia kama Mungu akinijalia ntapenda matibabu yawe bure.
SA: Malengo yako mazuri sana na bila shaka Mungu atakutangulia. Hongera sana.
Janeth: Asante na Mungu akubakiri kaka.
SA: Asante sana”
Janeth Pastor Mtonyi
Naam msomaji,
hapo ndio tumefikiwa mwisho wa makala hii. Asante sana kwa kufuatilia kuanzia
mwanzo. Usikose makala nyingine kali zaidi ya hii. Kila siku endelea kupitia
hapa. Kwa maoni, maswali au chochote, usisite kuwasiliana nasi kwa anuani ya moreinfoz@yahoo.com . Kwaheri kwa sasa.
Naona nia ya blog yako ni nzuri lakini hii itakua blog ya umbea..Wewe kutafuta watu wanaoishi ughaibuni ili iwe nini kujua maisha yao? Watu wamekaa kimya na maisha yao nyie kutwa kucha kuwatafuta. Mbona sisi hatuwatafuti nyie huko Africa tukawahoji mnafanya nini, mnakula nini etc. Hii ni umbea na hata sioni faida za hayo maswali unayowahoji, yatamnufaisha vipi mtu aliyeko Africa?
ReplyDeleteNa kama watu unaowahoji ni wafanyakazi ni nini kitanifanya nije nisome huku tena katika hii blog unless mimi ni mmbea nataka kujua maisha ya watu wengine la sivyo hutapata wasomaji wa maana wa blog yako....Na kama ni ndoto za kufanya mambo makubwa Africa kila mtu anazo.....Sasa sijui haya maswali yako yatamsaidia vipi mtu wa kawaida Africa.
Ningekushauri tafuta wajasirimali waliko ughaibuni ujue walihangaika vipi mpaka wakaweza kuwa na biashara katika hizi nchi za watu...kazi za kuajiriwa kila mtu anafanya huku ughaibuni na kulipwa mishahara mikubwa kuliko hata majudge Tanzania hilo ni jambo la kawaida kwa hiyo hamna jipya hapo lakini walioamua kujiajiri ndio itawasaidia hata huko nyumbani kupata idea za kujiajiri na sio kufikiria kazi ni kuajiriwa tu. Na pia walioko ughaibini wanaweza kujifunza moja au mawili ili nao waweze kujiajiri....Wajasirimali wako wachache lakini biashara zao ni big big na wengi wangefaidia na jisi walivyopitia mpaka wakajiajiri..kuajiriwa na kulipwa mishahara mikubwa hilo jambo la kawaida sana.....Just a friendly advice...
We soma tu kama wataka kumshauri muandkie mail ktk email yake na sio hapa
ReplyDeleteUshauri wako mzuri ila unakosea kuanza kukosoa hapa hewani, nadhani ushauri alotoa dada sara ndi uliotakiwa kuufuata, hainiingii akilini kwa mtu kama wewe tena unayeonekana msomi kuanza kuhoji wazi wazi, ulipaswa kumwandiki kwa email maana ameiweka wazi...acha ushamba, nyie ndio mnaoudisha harakati za watu nyuma.
ReplyDeleteDaima ukarimu huanzia nyumbani na siku zote nyumbani ni nyumbani japo hakuna mlo wala makazi.
ReplyDeleteWatanzania mliopata nafasi ya kwenda ughaibuni tunasubiri ukarimu wenu hapa nyumbani.Kumbukeni kuwa kutoa ni moyo na wala siyo utajiri na ukarimu wa mtoaji haupimwi kwa wingi au uchache wa matoleo yake.
Karibuni sana Tanzania kwenye ardhi ya mlima Kilimanjaro,visiwa vya Zanzibar,mbuga za Serengeti na daraja la kiuchumi na biashara kwa nchi za maziwa makuu kupitia bandari ya Dar es salaam.
HUNA UZALENDO WEWE NDUGU NDO MAANA HATA HUTAKI KUJITAMBULISHA HUFAI KATKA JAMIII NYIE NDO MNAO YUKAKANA KATIKA MITANDAO KWANI KUHOJIWA MTU NI VIBAYA KWANI UMEAMBIWA AMEMWOJI KUWA ANAMADAWA YA KULEVYOA ,KUWA MSTAARABU KAMA HUTAKI KUCHANGIA MAWAZO POTEZEA TUU TUACHIE WENYE KUSOMA MAMBO MBALIMBALI NYIE NDO MLIOSOMA HATA KIJIJINI KWENU HUJARUDI JAPO KUWAONA WALIOKUPA SAPOTI WAKATI UPO DARASA LA KWANZA NA HATA KAMA ULISOMEA FORODHANI DAR KUWA MSTAARABU BASI ,HONGERA DAA ACHANA NA HOA ENDELEA KUWAPA CHANGAMOTO HATA WALE WENZIO WANAOTAKA KUJA KUJENGA SHULE NAO WAJE
ReplyDeleteMIMI MTU KWAO
CHE JIAH