Monday, June 10, 2013

"Mtanzania Mmarekani" mwenye kusaidia "ufadhili" wa masomo ughaibuni

Leo katika mfululizo wa makala zetu, tunae mtanzania aishiye nchini Marekani. Huyu amekuwa na kiu ya muda mrefu kuwafanya vijana wanatimiza ndoto zao za kusoma nchi za Marekani au Ulaya,
Karibu kufuatilia mazungumzo yetu ya leo yanayobeba mada ya elimu ya ughaibuni…
“SA: Habari za siku kaka..
MAKULILO: Kwema kaka, naona leo umenizungukia, kuna jipya?
SA: “Haaaaaa! Haaaa! (Nikacheka kidogo) Kwa nini umesema hivyo kaka?
MAKULILO: Haaaa! Haaaa! (Akacheka pia) Nimependa sana harakati zako za kuwaunganisha Wanaafrika Mashariki. Hongera sana.
SA: Nakushukuru kwa kuutambua mchango wangu! Asante sana. Naomba ujitambulishe kwa wasomaji wetu kabla hatuaanza kuzungumzia mada yetu…
MAKULILO: Naitwa Ernest Boniphace Makulilo
SA: Kwa Afrika Mashariki, unatokea wapi?
MAKULILO: Natokea Tanzania, mkoani Kigoma.
SA: Uko nchi gani kwa sasa?
MAKULILO: Niko Japani kikazi, ila naishi San Diego, California, Marekani.
SA: Baada ya utambulisho huo, sasa naomba turejee kwenye mada yetu, unafanyaje kuwasaidia vijana wa Afrika Mashariki kusoma ughaibuni?
MAKULILO: Kwanza kabisa, niseme wazi kuwa, kusoma au kuishi ughaibuni, ni uamuzi wa mtu na inawezekana kwa kuamua na kupanga.
SA: Kuamua na kupanga kivipi?
MAKULILO: Namaanisha vijana wanatakiwa kujenga msingi mapema na kuamua kwa dhati kutoka moyoni kuja kusoma au kuishi ughaibuni.
SA: Lakini wakati mwingine inaweza kuwa ada kubwa katika vyuo vya ughaibuni, kama unavyojua maisha ya wengi Afrika Mashariki yalivyo magumu?
MAKULILO: Ni kweli usemayo, ndio maana mimi niliamua kuanzisha taasisi ya kusaidia kwa hilo…
SA: Unasaidiaje?
MAKULILO: Ninatafuta wafadhili na na kuweka taarifa zote wazi katika blog yangu, pia ushauri wa namna ya kupata ufadhili kwa njia ya rahisi sana.
SA: Unaposema kupata ufadhili kwa njia rahisi unamaanisha nini, kwani kuna njia ngumu?
MAKULILO: Hapo namaanisha, mwanafunzi ajitahidi kufuata maelekezo ya kitaalamu ktk kupata ufadhili, kwa mfano kama amedhamiria kupata ufadhili ndani ya kipindi cha mwaka fulani, basi aombe ufadhili katika vyuo zaidi ya kimoja ili kujiwekea nafasi nzuri zaidi..
SA: …Naona mazungumzo yetu yanazidi kuwa matamu, tunaomba ututajie namna unavyoweza kupatikana ili atakayehitaji akutafute kwa msaada zaidi.
MAKULILO: Vyema, napatikana katika blog http://makulilo.blogspot.com,  au kwa http://www.makulilofoundation.org
SA: Tunakushukuru sana na tunakutakia harakati njema.
MAKULILO: Asante sana kwa kufanya mahojiano nami na Mungu akubariki sana.”
Hivyo ndivyo tulivyozungumza na Mtanzania huyu mwenye nafasi kubwa sana ya kuwasaidia vijana kutoka nchi zinazoendelea, wenye ndoto za kusoma vyuo vya Ulaya na Marekani. Nawaomba msizitumie nafasi mnazozipata vibaya ili mziletee maendeleo ya kweli nchi zetu za Afrika Mashariki na siku moja maisha ya kutegemea misaada kutoka kwa wenzetu, yawe ndoto kuliko livyo sasa!
Tukutane tena, wakati mwingine kwa makala nyingine kali zaidi ya hii.
Kwa mawasiliano,usisite kuandika moreinfoz@yahoo.com

Ernest B. Makulilo katika pozi la kiutamaduni.

9 comments:

  1. Replies
    1. umeona eee!jamaa yuko juu ana moyo sana...@Sara J

      Delete
  2. Kazi nzuri hongera ...uandishi tofauti

    ReplyDelete
  3. Ama hakika ni jambo la busara mulilo li changia. Mola awabariki.

    ReplyDelete
  4. hongera sana kwa kuwa na mtazamo chanya

    ReplyDelete
  5. VIZURI SANA KAKA MKUBWA KWA KUTUSAIDIA NDUG ZAKO WA AFRIKA.NOVATUS G. NTABI

    ReplyDelete
  6. HONGERA NA ASNTE KAKA MKUBWA KWA KUTUSAIDIA NDUGU WA TANZANIA

    ReplyDelete