Idhaa ya Kiswahili ya CRI ilirusha matangazo yake
ya kwanza hewani kuanzia Tarehe Mosi, Septemba mwaka 1961 kutokana na
ushirikiano na juhudi kubwa za wafanyakazi wa China na wataalamu wa kigeni. Bw Ali
Miraji Mpatani, alikuwa miongoni mwa wataalamu waafrika waliokuja kusaidia
wakati idhaa hii ilipokaribia kutimiza mwaka mmoja. Mtaalamu Mpatani
alishirikiana bega kwa bega na wafanyakazi wa China na wanafunzi kadhaa
walioshiriki kazi ya idhaa hiyo kabla ya kuhitimu masomo, alitoa mchango
usiosahaulika katika kuiwezesha idhaa hii iendelee.
Matangazo ya idhaa hii ya kiswahili yanarushwa kila siku hewani kupitia masafa mafupi kuanzia saa 1:00 hadi 2:30 jioni; pia yanasikika nchini Kenya kupitia Idhaa ya kiswahili ya KBC saa 11:00 jioni kila siku; na yanarushwa hewani kwa kupitia Kampuni ya MIH ya Afrika ya kusini kuanzia saa 2:00 hadi 3:00 na kuanzia saa 5:00 hadi 6:00 jioni(saa za Afrika ya Mashariki).
Katika idhaa hii, kuna Taarifa ya Habari (kila siku), Maelezo Baada ya habari (Jumatatu hadi Ijumaa ), vipindi vya Wapenzi wa Michezo(Jumatatu), Nchi yetu Mbioni(Jumanne), Elimu na Afya (Jumatano), Tazama China (Alhamisi), Klabu ya Utamaduni (Jumamosi), Sanduku la Barua (Jumapili), Salamu Zenu (kila siku), Kuwa nami Jifunze Kichina (Jumanne na Alhamisi), Ijue China (Alhamisi) pamoja na Sayansi na Teknolojia (Jumatano).
Kuwatumikia wasikilizaji wake na kuongeza urafiki kati ya China na Afrika ni wajibu na jukumu la siku zote la Idhaa ya Kiswahili ya CRI. Matangazo ya idhaa hii yanalenga kusema ukweli na kuaminika, kujitahidi kuwawezesha wasikilizaji waielewe China na kuielewa dunia na kuwa ni kama daraja la urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika. Kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita, Idhaa ya Kiswahli ya CRI imeendelea vizuri na kupata mafanikio makubwa kutokana na uungaji mkono wa wasikilizaji wake, na huu umekuwa ni msingi wa kuandaa vizuri vipindi vinavyo wafurahisha wasikilizaji wake. Wafanyakazi wake wataendelea na juhudi kubwa na kutumia busara ipasavyo ili waweze kuboresha vipindi vyake.

Thanx za kutosha ziwaendee Radio China Kimataifa kwa kuandaa makala hii nzuri yenye ufafanuzi wa kutsoha kwa wasikilizaji.
Unaweza kuwasiliana nasi, kwa maoni au lolote kuhusiana na maisha ya Wanaafrika Mashariki waishio ughaibuni.
Tanzania na China ni wadau katika maendeleo na uchumi kwa miongo kadhaa lakini sina hakika iwapo CRI Idhaa ya Kiswahili ina redio washirika nchini Tanzania.Iwapo hakuna huu ni wakati ufaao kwa CRI kutafuta redio washirika itayowezesha matangazo yake yapate mashiko kama yale ya redio nyingine za kimataifa.
ReplyDeleteHONGERA CRI NA KARIBU TANZANIA KWENYE ARDHI YA MLIMA KILIMANJARO,VISIWA VYA ZANZIBAR,MBUGA ZA SERENGETI NA DARAJA LA KIUCHUMI KWA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM.
DeleteKwa kweli inawabidi hawa CRI wawe na washirika Tanzania kama ilivyo Kenya na nchi zingine
ReplyDeleteCRI wanakaribishwa kuwekeza Tanzania kama makampuni mengine ya kichina yanavyoendelea kufanya.Uwepo wa CRI nchini Tanzania utasaidia kukuza taaluma ya ukalima wa Kiswahili na Kichina kutokana na wingi wa wachina nchini Tanzania.Blogu hii ifuatilie kwa ukaribu uwekezaji huo wenye manufaa kijamii.
DeleteJe mzee wangu marehemu Haroub Miraj alijiunga nanyi mwaka gani? Kumbukumbu zinaonyesha alikuwa huko miaka ya sitini.
ReplyDeletehongera CRI ningependa kupata mawasiliano ili niweze kufanya mafunzo ya kujitolea kwa vitendo hapo china
ReplyDelete