Katika
mfululizo wa makala zetu, tutakuwa tukichambua na kudodosa maisha halisi ya
wanafarika mashariki waishio ughaibuni kwa kutazama uhalisia wao kuanzia
chakula, mavazi, malazi, kazi, nk. ili kujua tofauti ya maisha kati ya ughibuni
na Afrika Mashariki. Pia watakuwa wakitupa changamoto zinazowakabili ili kufikia
malengo yao.
Uwamahoro Phocus Irene,..ni kijana kutoka Rwanda. Huyu ndiye anayetufungulia mfululizo wa
makala zetu hapa. Kumbuka nchi ya Rwanda pia imejiunga katika jumuia ya Afrika Mashariki,
zaidi ya Kenya, Uganda na Tanzania zilizozoeleka. Karibu uungane nasi mwanzo
hadi mwisho wa makala.Mzungumzo ya leo yanafanyika kwa njia ya mtandao kama ifuatavyo:
SA:
Habari yako kaka!
Phocus:Nzuri
ndugu yangu habari za huko.SA: Huku ni salama…! Umebahatika kuwa Mwanaafrika Mashariki wa kwanza kufanyiwa mahojiano na mtandao huu unaozungumizia maisha yenu mlioko ughaibuni, unaizungumiziaje nafasi hii?
Phocus: Haa! Haaa! haaa! (anacheka), nimefurahi sana maana tangu mlivyotangaza imechukuwa muda kuanza na kwa kweli Mungu alikuwa akinitengenezea bahati hii ianzie kwangu! Asanteni sana.
SA:Asante kushukuru! Sasa naomba tuanze kwa kukufahamu kama hautajali,
Phocus: Kivipi?
SA:Jina lako kamili unaitwa nani?
Phocus: Asante, jina langu naitwa Uwamahoro Phocus Irene.
SA:Umezaliwa wapi na ni mwenyeji wa nchi gani kati ya nchi zinazounda jumuia ya Afika Mashariki?
Phocus:Mimi nimezaliwa nchini Rwanda katika mkoa wa Gisenyi, Rubavu.
SA:Unaweza kututajia mwaka wa kuzaliwa?
Phocus:Hapana kaka, umri ni siri yangu!
SA:Hamna shida kaka, hatuwezi kuingilia maamuzi yako maana ni haki yako hiyo, unaweza kutueleza uko nchi gani kwa sasa?
Phocus: Niko Canda.
SA: Mji gani?
Phocus:Montreal, Quibec.
SA: Uliingia nchini humo mwaka gani?
Phocus: Niliingia hapa mwaka 2007.
SA: Lengo kuu lilikuwa lipi?
Phocus: Nilikuja kusoma na sasa nimeshamaliza, niko kazini.
SA:Hongera sana kaka. Je, ni changamoto zipi unakabiliana nazo kila siku?
Phocus: Kwanza ni maisha mapya kwangu, japokuwa nimekaa kwa muda sasa, ila tamaduni za hapa na nyumbani ni tofauti.
SA:Unaposema tamaduni ni tofauti unamaanisha nini?
Phocus: Hawa wenzetu suala la kuvaa nguo nusu uchi hasa kwa mabinti ni jambo la kawaida kwao, so kwa mimi ilianza kunipa ugumu sana na sasa linaendelea kunitesa ila namwomba Mungu nizoee!
SA:Kabla hatujamaliza makala yetu fupi, una maoni gani kwa vijana wa Afrika Mashariki kuhusu maisha ya ughaibuni na mafanikio?
Phocus:Maoni yangu ni kwamba, yeyote anayepata nafasi ya kuja huku aje maana unafungua uelewa wako zaidi pia sio lazima kuja huku. Unaweza kubakia nyumbani na maisha yakaendelea tu.
SA:Ok, tunakushukuru kwa kutupatia muda wako wa kuzungumza na wasomaji wetu na tunaomba uwe balozi mzuri wa Swahili Abroad hapo mtaani kwako.
Phocus: Asanteni nanyi pia nawatakia mafaniko mema yenye Baraka tele! Mzidi kuwa wawakilishi wazuri na daraja bora kati ya Afrika Mashariki na watu wake wa ughaibuni..
SA: Asante.
Phocus:Asante.”
Naam, msoamji wetu hayo ndio yalikuwa mazungumzo kati yetu na Mwanaafrika Mashariki aishiye nchini Canada yaliyofanyika kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook. Iwapo ungependa kuzungumza nasi katika makala zetu zijazo, au una maswali au maoni, ushauri na lolote, usisite kuwasiliana nasi.
Asante kwa kutusoma na tunakutakia siku njema. Usikose makala nyingine na habari kila siku.
Uwamahoro Phocus Irene, katika pozi.
Nzuri sana, jamaa amejieleza vizuri, halafu mbona ameongea Kiswahili straight?amejifunzia wapi?
ReplyDeleteNdio dada Aisha, huyo jamaa ana uwezo mzuri wa kuzungumza lugha hii japo Wanyarwanda wengi wanashindwa kuitamka sawa sawa. Lakini ili kuleta ladha halisi tumejribu kuhariri baadhi ya maneno aliyokuwa anashindwa kuyatammka sawa sawa..
DeleteAsante kwa kutujuza na kweli tunajifunza mengi
ReplyDelete